Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Joshua Sanga akizindua Mafunzo ya zoezi la Mbinu Shirikishi na Harakishi la Chanjo ya Uviko-19 awamu ya pili amewataka wadau kuendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali kupitia vikao vya kamati za msingi za afya, kwenye Halmashauri, sambamba na kwenda kwa wananchi kufanya mikutano ya vijiji na Mitaa, kutoa ufafanuzi na maelekezo sahihi kwa baadhi ya makundi ya watu wenye imani potofu dhidi ya chanjo ya ugonjwa wa uviko-19.
Hata hivyo Timu za Uhamasishaji ziliweza kufanya vikao katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri kwa ajili ya kutoa Hamasa kwa wananchi ambapo makundi mbalimbali yalihusishwa wakiwemo Viongozi wa Dini, Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Watu Maarufu na Wenye ushawishi ndani ya Jamii, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wauguzi wa Afya kutoka Vituo mbalimbali vya Kutolea huduma lengo likiwa ni kutoa Elimu na Hamasa kwao ili Elimu ambayo wataipata wakaiambukize katika jamii na maeneo yao wanakoishi ,
Akaendelea kusema “Kuanzia tarehe 01 Oktoba 2021 wataalam wapite nyumba kwa nyumba na maeneo yenye mikusanyiko sokoni, stendi na sehemu zinazotoa huduma mbalimbali ikiwepo kwenye Misikiti na makanisa kwa siku za ijumaa na jumapili na kutoa huduma za chanjo kabla na baada ya ibada, huku wakizingatia namna rahisi ya utoajiwa chanjo kwa haraka bila ya foleni ili kurahisisha zoezi hilo.
Mwisho kabisa Kaimu Mkurugenzi amewataka wananchi wote katika Halmashauri ya WIilaya ya masasi na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo kuanzia tarehe 01 Oktoba 2021 itakuwa inapatikana katika Vituo vyote vya kutolea huduma yaani kuanzia ngazi ya zahanati zote, Vituo vya Afya, pamoja na Hospitali jambo ambalo litawezesha wananchi wengi kufanya kazi zao kwa uhuru bila ya woga wa virusi vya UVIKO-19 na kujenga Uchumi wa Familia zao na Taifa kwa Ujumla..
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mtwara ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Masasi kwa mapokeo mazuri ya chanjo ya UVIKO 19 katika mkoa huo, Mkoa wa Mtwara hadi kufikia siku ya leo umekuwa mstari wa mbele kwa kufikia asilimia 85 ya chanjo ya UVIKO 19 kati ya dozi 20,000 zilizokuwa zimepokelewa tokea Julai, 28,2021 kwenye Mkoa huo.
Amesema kuwa, katika kuhakikisha asilimia 15 za dozi zilizobaki zinakamilika fursa za chanjo zitolewe kwa wananchi hususani kwa maeneo ambayo yalibainika kuwa chini katika uchanjaji.
Katika kufanikisha zoezi hilo Gaguti amesisitiza kuwa, katika zoezi Shirikishi na Harakishi linalo endeshwa na Serikali kwa sasa, ni vizuri kila mtu ambaye bado hajajitokeza, aweze kujitokeza apate elimu na akielimika aweze kupatiwa chanjo ya UVIKO 19.
Pichani ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya akitoa neno juu ya zoezi la uchanjaji wa Uviko-19 wakati wa Mafunzo hayo kwa niaba ya Wizara yaliyolenga kuwajengea uwezo wauguzi wa Afya katika Vituo vya kutolea huduma mbinu shirikishi na Harakishi kwa wanachi dhidi ya chanjo ya Uviko-19 katika awamu ya pili.
Pichani ni Afisa Tehama wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Ndugu Shedrack Omary akitoa maelekezo kwa wauguzi wa Vituo vya Afya juu ya matumizi ya Mfumo wa kutuma Maombi ya Chanjo ya Uviko-19 ambapo maombi yote ya chanjo na taarifa mbalimbali zitakuwa zinafanyika kupitia mfumo huu ambapo muombaji atatakiwa kuwa na namba za kitambulisho kama vile kitambulisho cha mpiga kura, Nida, Passport, au Leseni wakati wa kuomba na mwisho wa zoezi muombaji atapata cheti maalumu ambacho ni Online certificate yenye Barcode ambacho kitamtambulisha Dunia nzima.Tuma maombi yako sasa kupitia link hii... https://chanjocovid.moh.go.tz/
Pichani ni washiriki wa idara ya Afya kutoka katika Vituo mbalimbali vya Kutolea Huduma katika Mafunzo Maalumu ya Mbinu Shirikishi na Harakishi dhidi ya Utoaji wa Chanjo ya Uviko-19 katika awamu ya pili.
Washiriki wa Semina elekezi juu ya Chanjo ya Uviko-19 wakiwa makini kusikiliza na kufuatilia hatua kwa hatua somo hilo, ambapo mada mbalimbali ziliweza kuwasilishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wauguzi wa Afya kutoka katika Vituo mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya Halmashauri ya Wilaya Masasi.
KORONA IPO NA INAUA TENA KWA KASI
CHUKUA HATUA NENDA KACHANJE LEO
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa