Zoezi la uchukuaji wa fomu kwaajili ya uteuzi wa Nafasi ya udiwani katika Uchaguzi mdogo wa kata ya Mnavira linaendelea vizuri baada ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Lulindi Beatrice Mwinuka Leo June 26,2023 kafanya ziara ya kutembelea na kukagua vituo vyote 12 ambavyo vimepangwa kutumika katika zoezi la kupiga kura ifikapo julai 13,2023 Amesema vituo vyote 12 amevitembelea na ameridhishwa kuona vipo katika Hali nzuri isipokuwa katika vituo vitatu Kati ya hivyo vinahitaji kutazamwa zaidi kwasababu vipo katika maeneo ya mashambani.Aidha akizungumzia hali ya uchukuaji fomu za uteuzi wa Nafasi hiyo ya udiwani, Mwinuka amesema licha ya zoezi Hilo kuanza June 24,2023 lakini hadi sasa hakuna chama chochote ambacho kimetoa mgombea wake na kwenda kuchukua fomu licha ya wengi wao kuhaidi kuwa kuanzia kesho June 27 watajitokeza kuchukua fomu hizo za uteuzi.hivyo ameendelea kuwaomba wananchi kupitia vyama vyao vya Siasa kushiriki kwa pamoja katika zoezi hilo muhimu la kumpata Kiongozi wao wa kata ambaye ndiye atakayewaletea Maendeleo ndani ya kata Yao.Mchakato huo unajiri baada ya Aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Ramadhan Chilumba kufariki Dunia kwa ajali ya pikipiki tarehe 15 Feb 2023.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa