Wishoni mwa mwezi June 2020, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ilipokea zaidi ya bilioni 3.4 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi 10, sekondari 5 na zahanati 10 lengo ikiwa kuwa na mzazingira mazuri ya utoleaji wa huduma.
Miundombinu hiyo ni pamoja na vyoo, madarasa, mabweni, mabwalo ya chakula na majiko kupikia chakula ambapo kwa shule za msingi zaidi ya shilingi bilioni 1.7 , shule za sekondari zaidi ya bilioni 1.6 huku zahanati 10 zikipata milioni 220 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Changwa Mkwazu kwenye kikao kazi cha kupokea maelekezo ya namna ya kutekeleza miradi hiyo, kwa wakuu wa shule, walimu wakuu, waratibu wa elimu kata, watendaji wa kata na vijiji pamoja na waganga wakuu kwenye maeneo yao.
Mkurugenzi aliwakumbushwa watuishi hao kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa kufuata mwongozo wa “force Account” ambao unataka kutumia mafundi wa kawaida yaani “local Fundi” na sio wakandarasi lengo ikiwa ni kupunguza gharama za ugenzi na kushirikisha jamii katia utekelezaji wa miradi.
Mkwazu ameeleza kuwa Halmashauri imepata fedha hizo kupitia program ya lipa kwa matokeo (EP4R) ambapo kwa mwaka uliopita halmashauri ilipata milioni 700 kupitia mpango huo “ simamieni vizuri miradi hii ili tuweze kupata fedha nyingi zaidi zitakazotuwezesha kuboresha huduma kwa wananchi wetu”.
Aidha, Mkwazu amewasisitiza watumishi hao kuzingatia kuunda kamati kama muungozo unavyoelekeza ambao viongozi wa eneo husika inaelekezwa wawe wajumbe “hali hii itasaidia utekelezaji wa miradi kuwa rahisi lakini pia kutekelezwa kwa ubora zaidi”.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa