Watumishi wapya wa kada mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakiwemo waalimu, wauguzi, waganga, watendaji wa kata na vijiji wapatiwa mafunzo elekezi ya awali katika utumishi wa umma lengo ikiwa kuwajengea uwezo wa namna ya kutekeleza majukumu yao katika utumishi wa umma.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Idara ya Utumishi na Utawala kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Utumishi wa umma za mwaka 2009, yalijikita zaidi kwenye muundo wa serikali za mitaa, Utawala Bora, maadili ya utumishi wa umma, haki za mtumishi wa umma, na sifa za mtendaji mambo ambayo ndi msingi wa utumishi wa umma
Aidha katika semina hiyo watumishi waya walipata ueewa juu ya usimamizi wa masula mabalimbali katika maeneo yao ikiwemo usimamizi wa miradi, utunzaji wa vyanzo vya maji na utunzaji wa mazingira na mambo mengine yanayofayika katika maeneo yao.
Ili kuepukana na migogoro mbalimbali katika watendaji wa vijiji walielezwa kuwa moja ya nyenzo ya kuzuia migogoro mbalimbali katika maeneo yao ni kutunga sheria ndogo ambazo zinatoa mwelekeo wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ikiwemo matumizi bora ya ardhi.
Watumishi hao pia walikumbushwa suala la maambuki ya ukimwi na magonjwa hivyo waliaswa kijikinga na maradhi hayo ili waendelee kuwa na afya njema na hivyo kufanya kazi zao kwa nguzu zote
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa