Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bibi Changwa M Mkwazu amewakumbusha wasimamizi wa vituo vya afya na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidii na weredi mkubwa huku wakizingatia maadili ya utumishi wa umma katika kutoa huduma kwa wananchi
Mkwazu ameyazungumza hayo leo kwenye kikao kazi kilicholenga kuwajengea uwezo wasimamizi wa vituo vya afya wa halmashauri hiyo juu ya masuala ya usimamizi wa rasilimali fedha katika vituo vya kutolea huduma za afya jambo ambalo limekuwa changamoto katika vituo vingi katika halmashauri hiyo.
Mkwazu alisema kuwa “kuna baadhi ya wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya wamekuwa na matumizi mabaya ya fedha zinazokusanywa kwenye vituo kwa makusudi au kwa kutojua taratibu za namna ya kuzitumia, natumai kupitia kikao hiki mtaweza kuelewa taratibu za kutumia fedha hizo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni zinavyoelekeza”
Aidha Mkwazu amesema baada ya kikao hicho cha kuwajengea uwezo juu ya usimamizi wa fedha na masuala mengine ikiwemo taratibu za manunuzi ya dawa, utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa sahihi, hatasita kumchukulia hatua za kinidhamu msimamizi wa kituo yoyote atakayetumia fedha za kituo vibaya kwani hata kuwa na cha kujitetea tena.
Mkwazu amewaomba watumishi hao kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia wananchi kwani kazi yao ni kubwa na inaguza uhai wa binadamu, hivyo huduma zisipotolewa vizuri wananchi wataendelea kuilalmikia serikali jambo ambalo serikali ya awamu ya tano haitaki litokee
“Naomba mbadilike Kuweni na moyo wa kuwasaidia wananchi walio na kipato cha chini, hivyo tuwe wazalendo, tuwajibike na kuwa hamu ya kuacha alama nzuri katika maeneo yetu tunayofanyia kazi” alisisitiza Mkwazu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa