Wanafunzi wa shule ya Sekondari Chidya iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefanya fujo na kusababisha uharibifu wa mali za shule na walimu wakidai walimu wanawabana sana kwenye masomo wakati wenyewe wanataka uhuru wa kutembea sio kuwa bize na masomo kila wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa akiwa na viongozi wengine wakitembelea madhara yaliyojitokeza wakati fujo zilizofanywa na wanafunzi shule ya sekondari ya chidya
Katika vurugu hizo wanafunzi walichoma pikipiki mbili, kuharibu vitu vyote ikiwemo tv, vitanda na vyombo vingine kwenye nyumba ya mwalimu wa taaluma pamoja na kuiba kuku 20 za mwalimu.
Kutokana na Vurugu hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa aliyefika shuleni hapo kujionea hali halisi, alieleza kuwa sababu iliyowafanya wananfunzi hao kufanya fujo inaonesha hawajitambui kabisa maana serikali itajitahidi kuboresha mazingira ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kuleta walimu lakini cha kushangaza wanasema wanafundishwa mno, ni jambo la ajabu sana.
Moja ya vifaa vilivyoharibiwa kwenye nyumba ya mwalimu
Akizungumza na uongozi wa shule hiyo pamoja na wanafunzi hao, Byakanwa alisema hatua za uchunguzi zinaendela na atakayekuwa amehusika kwa namna moja au nyingine hatua za kisheria zitachukuliwa ili iwe fundisho kwa wanafunzi wengine maana hatutawavumila wanafunzi wenye utovu wa nidhamu kiasi hiki.
Byakanwa aliwaeleza wanafunzi kuwa “Hatuwezi kutengeneza chidya ya wananfunzi wanaotaka kusikilizwa kila jambo hata kama halipo kwenye utaratibu, kama unataka uhuru wa kutokusoma ungebaki nyumbani lakini ukiwa hapa ni kusoma na si vingine na kama kuna tatizo liwasilishwe kwa utaratiibu sio kwa kufanya vurugu”
Byakamwa alisema kuwa “Kwa matokeao ya kidato cha sita mwaka jana hakukuwa na daraja sifuri, lakini hapa chidya naona mnajiandaa kuleta sifuri, sasa kabla hamjautia aibu mkoa wangu mtaondoka nyinyi kwanza”
Aidha Mkuu wa Mkoa amemwagiza Mkuu wa Shule hiyo ndugu Zawadi Mdimbe kuanzisha utaratibu wa kila mwananfunzi kuandika barua ya kuadihi kufuata sheria za shule ikiwemo utaratibu wa kufuata kuwasilisha malalamiko badala ya kufanya furugu ambazo zinasababisha hasara kwa mali na miundombinu ya shule.
Mkuu wa shule ya sekondari Chidya Zawadi Mdimbe (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo mbele ya viongozi walipotembelea shuleni hapo
Wakati serikali inajitahidi kuleta fedha za kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia ninyi mnafanya fujo kisa mnabanwa sana kwa kuwa bize na masomo, “ni ujinga ambao hauwezi kuvulimika jaribuni tena mtafutwa shule ili mjaribu ujinga maana elimu muona haifai” alisistiza Byakanwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Zawadi Mdimbe amesema vurugu hizo zilitokea usiku wa jumamosi ya tarehe 01 septemba 2018 na baada ya fujo wanafunzi 22 hawajarea shuleni mpaka sasa.
Shule ya sekondari chidya ilianzishwa mwaka 1923 ni kati ya shule kongwe ambazo serikali imetoa fedha zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya ukarabati lengo iiwa ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa