Kamati ya fedha Halmashauri ya Wilaya Masasi imemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi Shule ya Msingi Mkwaya (SHUU INVESTMENT) kuandika barua ya kuomba fedha Halmashauri ili aweze kukamilisha ujenzi huo haraka kabla ya tarehe 01 June 2024.
Kamati imetoa kauli hiyo mapema tarehe 06/05/2024 Katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Kamati ikiwa Katika Jimbo la Lulindi katika Kata ya Makong'onda, imefika Kijijini Mkwaya na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Mkwaya mradi ambao mwaka 2017 ulianza kwa kujengwa maboma manne na Ofisi kwa nguvu za Wananchi, na ujenzi wa umaliziaji maboma hayo umeanza tarehe 21/01/2024 huku mfumo unaotumika ni wa mkandarasi ambapo anatumia fedha zake mwenyewe na kazi ikikamilika ataomba kurejeshewa fedha zake baada ya Injinia Kutoa kibali cha kulipwa fedha hizo .
Hata hivyo Kamati imeshangazwa na mradi huo kukumbwa na changamoto mbalimbali na kubwa zaidi ikiwemo ni uletwaji wa vifaa vichachevichache hivyo kupelekea mradi kuchukua siku nyingi kukamilika, pia na uchache wa mafundi ambao wanaletwa na mkandarasi huyo katika mradi huo.
Aidha ifahamike kuwa kukamilika kwa mradi huo wa Shule ya Msingi Mkwaya kutawapunguzia Watoto mwendo wa kutembea umbali mrefu kufuata Shule hali ambayo inawadhoofisha sana kwenye taaluma kwani hufika Shule wakiwa wamechoka, Pia mradi huu ukikamilika utapunguza meundikano wa Wanafunzi darasani katika Shule ya Msingi Mango'nda ambayo inahudumia Vijiji vinne ambapo vijiji vitatu havina Shule kabisa.
Kazi iendeleeee......
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa