Baada ya Viongozi wa vyama vya msingi 100 waliokamatwa kufuatia ripoti ya uchunguzi ya madai ya malipo ya korosho ya wakulima wilayani masasi kwa misimu ya 2016/2017 na masimu wa 2017/2018 iliyowasilishwa tarehe 23.02.2018 wamerejesha jumla ya shilingi 1,277,935,540 kati ya 1,533,794,100 na 1,803,208,368 walizokuwa wanadai wakulima kulingana na bei kubwa na ndogo za minada .
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa mtwara mhe. Gelasius Byakanwa kwenye mkutano na wananchi katika kijiji cha Mwongozo kilichopo kata ya Nangoo halmashauri ya wilaya ya masasi ambapo alikwa anasikiliza kero ya wanachi hao ya kutolipwa fidia ya maeneo yaliathiriwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa mbwinji na kuwaeleza wananchi kuwa serikali inasikiliza na kutatua kero kwa haraka.
Mhe. Byakanwa serikali iliamua kuchukua hatua ili wakulima waweze kupata fedha zao lakini pia kuwafundisha viongozi wa vyama vya ushirika kuwa fedha za wakulima sio za kuzichezea kwa manufaa yao bali watekeleze wajibu wao kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa