Moja ya sababu inayopekelea umasikini katika jamii ni ongezeko la watoto kwenye kaya bila kuzingatia uwezo wa kuwapa mahitaji ya msingi ikiwemo chakula, afya na mengine. Ndio maana serikali kupitia wadau mbalimbali ya walianzisha huduma ya uzazi wa mpango ili kusaidia kupunguza vifo kwa akina mama wajawazito sambamba na kuboresha afya ya mama na mtoto.
Utoaji wa huduma bora za jamii kama elimu, miundombinu na huduma za afya zimakuwa zikilega lega kutokana na uwinao mdogo katia ya idadi ya watu na uwezo wa serikali.
Kutokana na sababu hiyo serikali kupitia taasisi ya Intrahealth imeaua kuoa elimuv ya uzazi wa mpango na faida zake katika kuleta maendeleo katika kaya na jamii kwa Wah. Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ili waweze kuwa mabalozi kwa wananchi katika kutekeleza mpango huu.
Uzazi wa mpango ni chachu ya kupunguza umaskini katika kaya (Household poverty) kwa kumwezesha mama kupata muda wa kushiriki shughuli za maendeleo, hupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 43 (43%) kulinga na tafiti zilizofanyika ambapo wajawazito 556 kwa kila vizazi hai 100,000 wako hatarini kupoteza maisha sawa na wajawazito 24 kila siku, na hutoa muda wa kutosha katika malezi na huduma (mavazi,shule n.k).
“Mkoa wa Mtwara Kwa mwaka 2014 – 2016 ulikuwa na vifo vya wajawazito 200, vifo 33 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi sawa na asilimia 17 (17%) ya vifo vyote,” alisema Ndg. Msafiri Swai mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka IntraHealth.
Wah. Madiwani mara baada ya mafunzo hayo wanatakiwa kwenda katika maeneo yao ya utawala na kuwahimiza wananchi kutumia njia ya uzazi wa mpango kulingana na mpango mkakati wa kitaifa wa huduma ya afya ya uzazi, watoto na vijana (OnePlan II ) wa mwaka 2016-2020 ili nyongeza ya watu iendane na uwiano wa rasilimali (ardhi) na huduma (elimu, afya, maji n.k).
“Ni asilimia 38% tu ya watanzania wanaaotumia njia za uzazi wa mpango, wakati lengo la Taifa ni kufikia asilimia 45 ifikapo mwaka 2020, Mpango wa kitaifa wa huduma za afya ya uzazi, watoto na vijana (OnePlan II) wa mwaka 2016 – 2020 unahimiza matumizi ya uzazi wa mpango wa muda mrefu .”alisema Msafiri Swai.
Uzazi wa mpango ni progamu mtambuka ya kimaendeleo na sio ya idara ya afya pekee, hivyo Wajumbe wa Halmashauri (Wah. Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo) wahakikishe fedha kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2018/19 na hususani upatikanaji wa vifaa vya njia ya kitanzi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa