Kuwa mshindi wa kwanza Kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofanyika Jijini Mwanza mwezi huu mwaka huu 2018 kwa timu ya wasichana ya mpira wa wavu (Volleyball) kutoka shule ya Msingi Mkalapa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara yatupe funzo viongozi, wazazi walezi na jamii kwa ujumla kuwa hakuna kinachoshindikana kama nia ya kufanya itakuwepo.
Timu ya volleyball wasichana shule ya masingi Mkalapa wakionesha mchezo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza kwa kuwa washindi wa kwanza kitaifa mashindano ya UMITASHUMTA 2018 iliyofanyika shuleni hapo
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe Chiputula Ibrahim katika sherehe ya kuipongeza timu hiyo kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA kwa mwaka huu na kueleza kuwa ushindi huo umeipa sheshima shule, jamii ya mkalapa hasa wazazi na walezi wa watoto, Halmashauri, Mkoa na Taifa kwa ujumla kwa viwango vyao vya uchezaji hivyo wananastaili pongezi za dhati kabisa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe Chiputula Ibrahim akihutubia wananchi na wananfunzi wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza kwa kuwa washindi wa kwanza kitaifa mashindano ya UMITASHUMTA 2018 iliyofanyika shuleni hapo
Chiputula aliendelea kueleza kuwa kuna baadhi ya wazazi wameendelea kuwa na dhana potofu kuwa michezo ni uhuni au kupoteza muda lakini kwa sasa dunia imebadilika michezo ni ajira, inaongeza chachu ya wanafunzi kupenda shule, ni afya lakini pia inampa fursa mwanafunzi kuongeza jografia kwa kukutana na watu tofatu katika mazingira mengine tofauti na nyumbani mambo ambayo yatamsaidia katika maisha yake ya baadae.
Timu ya wasichana 9 ya mpira wa volleyball iliyoshiriki michezo ya UMITASHUMTA mwaka 2018 na kuwa washindi wa kwanza kitaifa kati yao sita wako darasa la saba katika hafla fupi ya kuwaongeza kwa ushindi huo
“Timu hii inaundwa na wasichana 9 walioshiriki mashindano haya, leo tunawapongeza kwa kuwapata zawadi mbalimbali, tukio la leo liwape chachu wazazi wengine kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye mazoezi ya michezo mbalimbali ili kuwapa fursa ya kujifunza maana michezo ni sehemu ya masomo ambayo wakiyazingatia yatawasaidia kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa” alisisitiza Chiputula.
Wananchi na wananfunzi wakiwa kwenye hafla fupi ya kuipongeza timu ya volleyball iliyopata ushindi wa kwanza kitaifa
kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo Elizabeth Mlaponi alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikicheza vizuri kwa muda sasa lakini kadri miaka inavyoenda kinafanya vizuri zaidi kutokana na juhudi anazozifanya Kocha wa mchezo huo ndugu Gabriel Joshua ambaye anajitolea kuwafunsisha wanafunzi, kama Halmashauri tunampongeza sana maana yeye ndio chanzo cha ushindi huu.
Kocha wa timu ya volleyball kituo cha Mkalapa Gabriel Joshua akipeana mkono na Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Elizabeth Mlaponi baada ya kupokea zawadi kwenye hafla fupi ya kuiwapongeza timu ya wasichana iliyopata ushindi wa kwanza kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA 2018
Aidha Afisa elimu amewaasa wazazi wote kuto katisha ndoto za watoto wao kwa kuwawambia wafanye vibaya kwenye mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi ambayo itafanyika mwanzoni mwa mwezi wa tisa maana tabia hiyo inafanywa na baadhi ya wazai kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo linawanyima watoto haki ya kupata elimu.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Elizabeth Mlaponi akitoa neno kwenye hafla fupi ya kuiwapongeza timu ya wasichana iliyopata ushindi wa kwanza kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA 2018
Mlaponi amewaasa wazazi wenye tabia ya kuwashawishi wanafunzi kutofanya vizuri mitihani yao ya kumaliza elimu ya msing kwa kusema kuwa “kwa maisha ya sasa elimu ni kila kitu hata kwenye michezo elimu pia inatakiwa hivyo waachenoi watoto wafanye mitihani yao vizuri ili waendelee na elimu ya sekondari kwani serikali inatoa elimu bila malipo hivyo acheni tabia hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla”
Kwaya ya wanafunzi wa shule ya masingi Mkalapa wakitumbuiza wakati wa hafla fupi ya kuiwapongeza wanafunzi wenzao walioshiriki mchezo wa volleball na kuwa washindi wa Kwanza kitaifa
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wa watoto walioshiriki mashindano hayo bibi Amina Lukas alieleza kuwa amejisikia vizuri mtoto wake kuwa sehemu ya ushindi huo, lakini pamoja na kushinda mtoto wake pia amekuwa na nidhamu, anajituma katika masomo maana michezo inamwongezea umakini katika kufanya kila jambo.
Walimu wa shule ya masingi Mkalapa wakiwa kwenye halfa ya kuwapongeza wanafunzi wao kwa ushindi waliopata.
“Namshukuru mwalimu anayewafundisha kwa kweli anawasaidia watoto na mimi kama mzazi namuruhusu kila siku kwenda kwenye mazoezi lakini pia namshauri kuzingatia masomo darasasni kwani michezo inaenda sambamba na kufanya vizuri kwenye masomo” alisema Amina.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa