Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inaendesha zoezi la kukusanya taarifa za wakulima wote ikiwemo zao la korosho lengo ilikwa ni kujenga kanzi data (Database) ya Wilaya na hatimae kuwa na takwimu za wakulima kwa mkoa mzima wa Mtwara kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo utoaji wa pembejeo.
Zoezi hilo litaendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia tarehe 24 hadi 30 aprili ,2018 ambapo kila mkulima atapaswa kujaza fomu hiyo inayompa fursa mkulima kueleza ukubwa shamba, idadi ya mikorosho midogo na mikubwa pamoja na kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula.
Akiongea kwenye kikao elekezi kwa watendaji wa vijiji Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya masasi ndugu Winfrid Tamba alieleza kuwa, taarifa hizo za wakulima zitasaidia kupata takwimu sahihi za mahitaji ya pembejeo, ukubwa wa maeneo yanayotumika kuzalisha mazao na matarajio ya mavuno pamoja na kuondoa biashara haramu ya Kangomba.
Tamba alisema kila Mkulima anatakiwa ajaze nakala mbili za fomu ambapo Fomu moja itabaki kwenye ofisi ya kijiji ambako shamba lake lipo, na fomu nyingine itapelekwa ofisi ya Halmashauri (idara ya kilimo) kwa ajili ya kumbukumbu.
“Zoezi hili ni muhimu sana, ni vema kila mkulima ajaze fomu hizi kwa kuwa zoezi ni la muda maalum” alisema Tamba. Lakini zoezi hili litakuwa endelevu kwa wakulima wapya
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa