Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara GELASIUS BYAKANWA leo tarehe 23.12.2020 alitembelea Masasi katika Halmashauri ya Mji Masasi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya masasi na kupata fursa ya kutembelea tarafa ya Lisekese katika kata ya Namatutwe pamoja na kata ya Nanjota na kufanya Mkutano na wananchi juu ya maendeleo na utekelezaji wa kampeni yake aliyoiyanzisha hivi karibuni yenye kaulimbiu ijulikanayo kama KAMPENI YA ONDOA MAPORI ONGEZA UZALISHAJI WILAYA YA MASASI na kupokea taarifa ya wilaya na Halmashauri kwa ujumla ambayo ilisema,
Wilaya ya Masasi ina jumla ya hekta 280,696 zinazofaa kwa kilimo ambapo kati ya hizo Halmshauri ya Wilaya ina hekta 280,468.5 zinazolimwa kwa sasa ni hekta 184,935.5 sawa na asilimia 65.93. Halmashauri ya mji ina eneo linalofaa kwa kilimo lipatalo hekta 227.5 na zinazolimwa kwa sasa ni hekta 90 sawa na asilimia 40. Mazao ya kipaumbele ya biashara ni korosho, ufuta, alizeti, mbaazi, karanga na choroko. Aidha mazao ya chakula ni muhogo, mahindi, mpunga, mtama na mboga mboga.
Wilaya ya Masasi inakadiriwa kuwa na miti ya mikorosho ipatayo 4,868,365 ambapo Halmashauri ya Wilaya ina mikorosho 4,044,002 na Mji ina mikorosho ipatayo 824,363
Uzalishaji wa korosho umeendelea kushuka kwa takribani miaka mitatu kuanzia msimu wa 2017/2018 hadi 2020/2021. Hata hivyo uzalishaji wa ufuta umeendelea kuongezeka kuanzia msimu wa 2018/2019. Pamoja na ongezeko hilo la uzalishaji, Wilaya ya Masasi imejipanga kuongeza uzalishaji kwa kuendelea kutao hamasa kupitia mikutano mbalimbali, vikundi na mkulima mmoja mmoja kwa kuanzisha mashamba mapya yenye kufuata kanuni bora za kilimo.
Mtaalamu wa kilimo kutoka Taasisi ya kilimo ya Naliendele Mkoani Mtwara akiwaonyesha na kutoa Elimu kwa wananchi namna bora ya kukata mikorosho iliyozeeka kwa lengo la kubebesha mikorosho ya kisasa ambayo itawaleatea tija zaidi na kuinua kipato cha WANANCHI.
Sikiliza hotuba kamili ya mkuu wa Mkoa wa mtwara kwenye link hapo chini
Wananchi wakiwa wamekusanyika wakifuatilia kwa ukaribu namna miti mizee ya mikorosho inavyoweza kukatwa kwa kutumia cheinisoo na kuendelea kupata Elimu ya namna bora ya kubebesha mikorosho mipya kwa njia ya kisasa ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji na kuondokana na kilimo cha mazoea.
Kwa taarifa zaidi unaweza kupakua taarifa ya Wilaya, Taarifa ya kata ya Namatutwe, na taarifa ya kata ya Nanjota pamoja na hotuba ya mkuu wa mkoa kwa njia ya sauti
TAARIFA YA WILAYA2020 kampeni mapori.pdf
TAARIFA YA KATA YA Nanjota.pdf
TAARIFA YA KATA YA Namatutwe..pdf
http://www.masasidc.go.tz/storage/app/media/AUDIO%20HOTUBA%20MKUU%20WA%20MKOA.mp4
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa