Dr.Paul Amanieli Chikira aliyesimama kulia ambae ni Mshauri katika masuala ya utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi kwa kanda ya kusini akitoa mafunzo kwa watendaji wa kata na Vijiji Serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3+) katika awamu ya pili.
Serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3+) katika awamu ya pili unaofadhiliwa na shirika la mandeleo ya kimataifa la marekani (USAID) imetoa mafunzo kwa wakuu wa idara na vitengo pamoja na watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi katika ukumbi wa mikutano uliopo mbuyuni.
Akizindua semina hiyo Dr.Paul Amanieli Chikira ambae ni Mshauri katika masuala ya utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi kwa kanda ya kusini alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watendaji kuweza kutekeleza afua zinazohusu ushirikishwaji wa wananchi katika masuala mbalimbali ya utawala bora, mipango na bajeti katika ngazi mbalimbali hivyo kupitia mafunzo haya alisema yataweza kuwajengea uwezo watumishi wa ngazi zote kufanya kazi zao vizuri kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na serikali pamoja na kuwatumikia wananchi wa ngazi za chini kwa weledi
Pia amesisitiza juu ya matumizi ya Redio jamii,Tovuti na vyombo vingine vya mawasiliano vinavyopatikana katika maeneo yetu vitumike ipasavyo katika kuhabarisha umma juu ya matukio na masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa pia ndani ya Halmashauri yetu
Mwezeshaji Peter Mushi Afisa Maendeleo ya jamii akitoa neno kwa wahiriki wa mafunzo ambao ni watendaji wa kata na Vijiji katika semina iliyoandaliwa na Serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za Umma (PS3+) katika awamu ya pili.
Washiriki wa semina iliyoandaliwa na ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3+) kutoka kata na vijiji mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi wakiwa makini kumsikiliza mwezeshaji katika ukumbi wa mikutano uliopo Mbuyuni.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa