Shule za Msingi Nakachindu na Chipango zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara zilizokuwa na hali mbaya ya miundombinu ikiwemo madarasa na vyoo zitaondokana kabisa na upungufu wa miundombinu hiyo baada ya serikali ya Japani kupitia shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania life improvement association (TALIA) kujenga madarasa 7 na matundu ya vyoo 12 katika shule hizo kwa gharama ya shilingi milioni 182.
Ujenzi wa Jengo la madarasa matatu katiaka shule ya msingi Chipango kwa msaada wa Serikali ya Japani kwa kushirikiana na Shirika la TALIA
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu alisema kuwa Halmshauri ina upungufu mkubwa wa miundombinu ya madarasa, vyoo na nyumba za walimu hivyo msaada huu ni mkubwa sana hasa kwenye shule hizi mbili ambazo ziliuwa na hali mbaya sana.
Mkwazu alikiri kuwa “Shule ya Nakachindu ilikuwa na madarasa mawili tu Halmashauri mwaka jana ilijenga darasa moja yakawa matatu lakini bado haikukidhi mahitaji ilikuwa ni wakati mugumu kwa walimu na wanafunzi maana iliwabidi wanafunzi wa madarasa tofauti kusoma katika darasa moja”
Ujenzi wa madarasa haya utamaliza kabisa upungufu wa vyumba vya madarasa na vyoo katika shule hizo kwani kila darasa litakuwa na chumba chake tofauti na hapo awali ambapo wanafunzi wa madarasa tofauti walitumia chumba kimoja kusomea.
Aidha Mkwazu ameishukuru Serikali ya Japani na shirika la TALIA kwa kuweza kuona uhitaji mkubwa wa miundombinu ya shule na kuamua kusaidia ujenzi wa madarasa 7 na vyoo matundu 12 ya kisasa kabisa katika shule za Nakachindu na Chipango kwani serikali pekee haiwezi kumaliza tatizo hilo
Kwa upande wake msimamizi wa mradi kutoka Ubalozi wa Japani nchini Tanzania Mai Yamazaki alisema kuwa umekuwa ukichangia fedha katika miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta ya Afya, elimu na maji tangu mwaka 1991 lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za jamii kwa wananchi.
Mwakilishi wa ubalozi wa Japani nchini Tanzania (wa kwanza kulia) akitoa maelezo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Nakachindu
Mai alifafanua kuwa “ miundombinu ya madarasa na vyoo inayojengwa katika shule hizi ni ya kisasa kabisa ambapo itakuwa na madilisha ya vioo, umeme na yataezekwa kwa mabati ya kisasa, lengo ni kuyafanya mazingira ya shule kuwa mazuri lakini pia wanafunzi kuwa na mazingira bora ya kusomea”
Nae Kaimu Afisa Elimu Msingi ndugu Eugine Ngaeje alieleza kuwa Halmashauri iliainisha shule zenye matatizo kwa shirika la TALIA na kufanya ukaguzi katika shule hizo, ndipo shule za nakachindu na chipango zikakaonekana kuwa na shida kubwa zaidi “ tunawashukuru sana kwa msaada wao maana umeondoa kabisa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na vyoo, tunategemea walimu na wananfunzi watakuwa na mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia.
Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nakachindu Fortunatus Nichelewa ameishukuru serikali ya Japani na shirika la TALIA kwa kuweza kukubali kutoa fedha za ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule yake kwani shule ilikuwa na madarasa matatu tu lakini baada ya kukamilika hakutakuwa na upungufu tena.
Mwakilishi wa ubalozi wa Japani nchini Tanzania (wa katikakti) akitoa maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa H/W , wawakilishi wa shirika la TALIA na watumishi wengine wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Chipango
Nichelewa alieleza kuwa “hali ilikuwa mbaya sana wanafunzi wa madarasa yote kutumia vyumba vitatu vya madarasa, chumba kimoja wanatumia wanafunzi wa madarasa matatu hali ambayo ilipelekea usikivu kuwa mdogo sana”
Halmashauri ya wilaya ya masasi ina upungufu wa madarasa 802 , matundu ya vyoo 582 na nyumba za walimu 1206 kwa upande wa shule za msingi
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa