Juni 5 kila mwaka, ni siku ya maadimisho ya mazingira duniani hivyo nchi yetu huungana na mataifa mengine duniani kuhadhimisha siku iyo, lengo ikiwa ni kuendelea kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira
Mabadiliko ya tabianchi husababishwa na mfumo wa mazingira wa asili na mfumo wa maisha ya binadamu, mabadiliko hayo hupelekea changamoto mbalimbli katika maendeleo. Changamoto hizo ni pamoja na ukame, ongezeko la joto, mafuriko na vimbunga.
Kauli mbiu ya siku ya mazingira kwa mwaka huu 2020 ni “tuhifadhi mazingira kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi” Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kama maeneo mengine yanayokumbwa na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo upungufu wa mvua, hali inayopelekea uzalishaji mdogo wa mazao ya chakula na biashara na Kukauka kwa vyanzo vya maji.
Kutokana na uhalisia huo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya mwaka huu inayosema“tuhifadhi mazingira kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi” kwa kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa umma kupitia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari (radio za kijamii, mitandao ya kijamii na tovuti ya halmashauri) pamoja mbao za matangazo.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kupitia Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) inatarajia kupanda miti 450 katika maeneo ya vyanzo vya maji vya chiwambo na Liputu ikiwa ni sehemu ya kutekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka huu inayosisitiza utunzaji wa mazingira.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa