Wakati tunasherekea siku ya wananwake duniani huku wananwake wakiwa wamepiga hatua kimaendeleo kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi lakini watoto wa kike nao hawako nyuma katika kushiriki maendeleo haya kupitia vipaji vyao
Hiyo imedhihirishwa na timu ya volleyball ya watoto wa kike kutoka shule ya msingi na sekondari Mkalapa zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakicheza mchezo wa volleyball siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa katika Kata ya Ndanda kuonesha uwezo wao kucheza mchezo huo maarufu duniani kwa kiwango cha juu.
Timu ya watoto hao ni timu ambayo imeupa ushindi Mkoa wa Mtwara katika mashindano ya Umiseta na umitashumta, hivyo watoto wa kike wakiwezeshwa wananweza katika kujitelea maendeleo lakini pia kushiriki katika safari ya kuelekea uchumi wa Viwanda kwa kutumia vipaji vyao.
Tukumbuke kuwa kila mwanamke alianza kuwa mtoto hivyo tuwasaidie watoto wawe wanawake bora wa baadae kwa kuendeleza vipaji vyao na kuwapa elimu bora.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa halamshauri ya wilaya ya masasi ambaye pia ndiye kocha wa timu hiyo ndugu Gabriel Joshua alisema kuwa watoto wana vipaji mbalimbali ambavyo vikiendelezwa vitawasasidia katika maisha yao lakini pia kuwajengea ujasiri wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia vipaji vyao.
Joshua amesema kuwa “nafundisha wanafunzi wa shule hizi mbili msingi na sekondari wakike na wakiume lakini timu ya watoto wa kike ni bora zaidi na inauwezo wa kushindana kitaifa hivyo kama walimu na wazazi tutatambua vipaji vya watoto na kuviendeleza ni namna pekee ya kuwawezesha kufikia uchumi wa viwanda”
Katika sherehe hizi watoto wameonesha michezo tofauti kwa hisia kabisa hali inayoashiria kuwa wakiendelezwa watakuwa wabobezi wazuri kwenye fani zao.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa