Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya Masasi imesema inaendelea kufanya ufuatiliaji ili kuwabaini wale wote ambao wanajihusisha na wizi wa mafuta (diesel) katika eneo ambalo limeanza kutekelezwa mradi wa ujenzi wa barabara kutokea Newala - Masasi na hasa katika eneo la Msanga, Mitesa hadi Nagaga.
Mhe.Lauteri John Kanoni ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa imeonekana wezi hao kwa asilimia kubwa sio wenyeji wa maeneo hayo bali wapo wahamiaji ambao wamefika kwenye Vijiji hivyo kumbe ni wezi wazoefu ambao wamezoea kuiba mafuta kwenye miradi huko walikotoka.
Amesema "Lakini kwenye maeneo yetu watu wamekuja wamepanga majumbani na tunaishi nao ndio wanaofanya huo wizi, kwaiyo niombe Watendaji wa kata, waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Vijiji nendeni mkawatambue watu ambao wapo huko wamekuja kwa Shughuli zipi, Lakini Kama Kuna wenyeji basi tuwatahadharishe hii sio dalili nzuri, na sisi kupitia vyombo vyetu vya dola tutaendelea kufanya ufuatiliaji tutawakamata" alisema
Ameongeza kuwa kwasasa tayari vifaa vingi vya ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo mitambo, magari n.k vimeanza kuletwa hii ikiashiria sasa ujenzi huo unakwenda kutekelezwa kwa kasi zaidi.
Na: Winifrida Ndunguru.
..@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa