KAMATI YA FEDHA YAIPONGEZA HALMASHAURI YA KIJIJI NAKARARA - KUFANIKISHA MRADI WA VYOO MATUNDU 10.
Kamati ya fedha Halmashauri ya Wilaya Masasi imeipongeza Halmashauri ya Kijiji Cha Nakarara, iliyopo katika Kata ya Makong'onda kwa kushiriki kikamilifu katika Shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa matundu 10 ya vyoo Katika Shule ya Msingi Nakarara.
Kamati imetoa pongezi hizo katika muendelezo wake wa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ambapo katika Shule ya Msingi Nakarara jumla ya kiasi Cha Fedha ikiwa ni Ruzuku ya Serikali shilingi milioni 11,000,000.00 zilipokelewa kwa nyakati tofauti zikilenga ujenzi wa mradi wa vyoo Katika Shule ya Msingi Nakarara, ambapo awamu ya Kwanza tarehe 01/07/2023 shilingi milioni 8,000,000/= na tarehe 01/03/2024 wamepokea shilingi milioni 3,000,000/=
"Mimi niwapongeze sana Kamati, mradi umetekelezwa vizuri, chamsingi kwamba yale matarajio tunayoyataka yawe Kweli kwa maana ikiwemo Milango iwekwe haraka ili Wanafunzi waanze kuvitumia vyoo hivyo, huku tukiangalia Namna nyingine ya kuongeza matundu mengine ya vyoo kwa ajili ya wavulana." Alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Ndg.Ibrahimu Chiputula.
Edga Erio ni Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Nakarara akisoma taarifa ya mradi na utekelezaji wake mbele ya Kamati hiyo fedha amesema, hatua ya mradi huo hadi sasa tayari matundu 8 yapo katika hatua za mwisho za umaliziaji na matundu 2 kazi imeanza ya kufuatilia vifaa na Eneo la ujenzi limeandaliwa huku ujenzi huo ukitarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi may
Amesema mafanikio hayo ni kutokana na ushirikiano mzuri wa wajumbe wa Kamati na Wananchi kushiriki kikamilifu Shughuli za kijamii, Ushirikiano wa viongozi wa Serikali na uongozi wa Shule na kata, ushirikiano wa Viongozi wa Serikali na wakuu wa Idara.
Hata hivyo pamoja na kuelezea mafanikio hayo Lakini pia akatumia fursa hiyo kuzitaja changamoto zingine zinazoikabili Shule hiyo ikiwemo vyoo bado ni tatizo kulingana na idadi ya Wanafunzi waliopo kwasasa hivyo yanahitajika matundu mengine ya vyoo 25, chumba kimoja Cha Darasa na Ofisi ya Mwalimu mkuu pamoja na uhitaji wa Waalimu watano.
Shule ya Msingi Nakarara ina jumla ya Wanafunzi 634, Wavulana wakiwa ni 318 na Wasichana ni 316.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa