HOSPITALI mpya ya Wilaya ya Masasi mkoani MTWARA iliyojengwa na serikali katika kijiji cha Mbuyuni kata ya Mbuyuni kwa gharama ya zaidi ya bilioni 1.5 imeanza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi wa Halmashauri hiyo leo tarehe 13.07.2020 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu kwa awamu ya kwanza. Tukio hili limeudhuriwa na wananchi wa kata ya mbuyuni, viongozi wa dini viongozi mbalimbali wa serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Bi Changwa M. Mkwazu wakati wa uzinduzi wa utoaji wa huduma ya Hospitali
Huduma hizo zimezinduliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi Changwa M. Mkwazu ameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo akisema itaboresha huduma za afya kwa kiwango kikubwa.
Mkwazu ameeleza kuwa, jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika kukamilisha miundombinu na serikali imeongeza jumla ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya kumalizia miundombinu ya maji na umeme. “ tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa kutuletea fedha za ujenzi wa hospitali ya wilaya na leo watu wanaanza kupata huduma”
Aidha Mkwazu, amewashukuru wananchi wa kata ya mbuyuni kwa kutoa ardhi yao bure kwa ajili ya ujenzi wa hospitali lakini pia ushiriki wao kwa muda wote wa utekelezaji wa Mradi “asanteni sana”
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Mbuyuni, mwenyekiti wa kijiji cha mbuyuni alisema kuwa “ tunaishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa ufanikisha ujenzi wa hospitali ya wilaya katika kijiji chetu, “ si ni jambo kubwa kulala na zahanati na kuamka na hospitali ya Halmashauri, salamu zimfikie Mhe Rais na viongozi wote kwa kazi iliyotukuka”
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano Halmashauri ya wilaya ya masasi imefanikiwa kujenga Hospitali moja, vituo vya afya viwili, ujenzi wa wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Chiwale na uboreshaji wa Zahanati mbalimbali
wananchi wa Mbuyuni wakati wa uzinduzi wa utoaji wa Huduma katika Hospitali ya halmashauri leo tarehe 13.07.2020
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa