Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi limefika ukomo wake leo rasmi tarehe 10 Juni, 2020 tangu lilipoaanzishwa rasmi tarehe 10 Desemba, 2015.
Akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani la kupokea taarifa ya ukomo wa madaraka ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri hiyo, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee amewapongeza madiwani kwa ushirikiano walioonesha katika kusimamia shughuli za maendeleo kadri walivyoweza katika kipindi chote cha uongozi wao.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee (aliyesimama) akitoa nasahaa wakati wa mkutano maalumu wa ukomo wa maraka ya madiwani tarehe 10 juni,2020
Aidha amewatakia kila la heri kwa watakaoingia kwenye kinyang'anyilo cha udiwani katika uchaguzi ujao na kuwakumbusha kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake mhe Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Satmah amewaeleza wajumbe kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 129.13 ambapo jumla shilingi 2,898,063,619.08 zimekusanywa kati ya shilingi 2,244,382,000 zilizokadiriwa kukusanywa. "Hii ni sawa na ongezeko la 29.13% tunastahili kujipongeza kwa mafanikio haya"
Satmah aliendelea kufafanua kwa wajumbe kuwa Halmashauri imetekeleza miradi ya sekta mbalimbali kupitia vyanzo mbalimbali cha mapato mfano" kwa idara ya msingi tumefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 126, vyoo matundu 660, nyumba za Walimu 9 na madawati 1674"
Kwa upande wa sekondari, miundombinu ya mabweni ,madarasa 45 maabara 3 vyoo matundu 270, nyumba za watumishi 13 imejengwa pamoja na kutengeneza viti 980 na meza 904 lengo ikiwa ni kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Iadha kwa upande wa afya huduma zimeendelea kuboreshwa ambapo kwa kipindi cha miaka 5 tumefanikiwa kupanua vituo vya afya 3, ujenzi wa zahanati 7 pamoja na ujenzi wa hospitali ya Halmashauri eneo la Mbuyuni.
mhe Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Satma akiwasilisha taarifa kwa Wajumbe kwenye mkutano maalumu wa ukomo wa maraka ya madiwani tarehe 10 juni,2020
Aidha, Satmah amewapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa ushirikiano walioonesha wakati wote wa uongozi wao pamoja na uvumilivu wa kufanya kazi bila kupata stahiki zao kwa muda wa Miesi 18 hali iliyosababishwa na upungufu wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
"Ni vizuri kubuni vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea ushuru wa korosho pekee ili tatizo kama hilo lisijitokeze tena kwa waheshimiwa madiwani watakaofanikiwa kurudi baada ya uchaguzi"
Nae Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bibi Changwa Mkwazu amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa ushirikiano walioonesha kwa kipindi chote cha uongozi wao kwani kwa pamoja wameweza kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha za serikali hali ilipelekea halmashauri kupata HATI safi katika kaguzi mbalimbali za hesabu za serikali.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa