Mh. Mkuu wa Wilaya ya Masasi akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi iliyopo katika kata ya Mbuyuni.
Mkutano wa Robo ya Nne 2020/2021 wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilayani Masasi umehitimishwa mapema leo katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Mbuyuni kata ya Mbuyuni, Katika Mkutano huo,Taarifa za Kata 34 za Halmashauri ya Wilaya ya masasi zimewasilishwa na kujadiliwa kwa kina pamoja na wataalamu wa idara na vitengo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya wilaya ya masasi pamoja na Taasisi nyingine kama vile Takukuru,Tarura,Bila kusahau Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwa ajili ya kujibu hoja mbalimbali za waheshimiwa madiwani kwa niaba ya wananchi kwa ujumla.Ambapo waheshimiwa madiwani waliweza kuhoji maswala mbalimbali yanayohusu wananchi wao likiwemo tatizo la wakulima na wafugaji, katika maeneo ya mpakani kama vile chikoropola uhaba wa watumishi hasa katika Idara ya Mifugo,pamoja na Huduma ya Bima ya Afya kwa wananchi yaani CHF Iliyoboreshwa ambapo Meneja wa Bima Mkoa aliwaeleza waheshimiwa madiwani kuwa wana mpango wa kuzindua Huduma mpya ya Bima ijulikanayo kama Mafao ya Vifurushi vya Bima kwa wananchi ikiwa huduma hiyo itampa fursa mwananchi mojamoja kuweza kulipia huduma ya Bima kadili anavyoweza.
.Madiwani katika Taarifa zao wameelezea Ujenzi mbalimbali wa miundombinu unaoendelea katika Kata zao ikiwemo Ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, zahanati, vituo vya Afya, miundombinu ya maji, na vyoo. Aidha, wametoa pongezi za dhati kwa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kupeleka fedha za miradi vijijini katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji pamoja na mawasiliano.
Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye kikao cha kufunga mwaka wakionyesha umakini mkubwa wa kusikiliza na kufuatilia hoja mbalimbali zinazotolewa na wadau mbalimbali katika kikao hicho.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa