Halmashauri ya wilaya ya Masasi Kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii, haina mamlaka ya kusajili NGO’S hivyo usajili wa NGO’S hufanyika Wizarani ofisi ya Maendeleo ya jamii, mbrella au Wizara ya mambo ya ndani.
NGO’S ambayo inahitaji kufanya kazi na H/W ya Masasi ni lazima kufanya yafuatayo.
Kuwasilisha Barua ya kuomba idhini kwa Mkurugenzi ya kufanya kazi kwenye Halmashauri pamoja na kuonesha mipango na malengo yake na maeneo ya mradi. Barua hiyo iambatane na barua toka kwa Katibu Mkuu TAMISEMI inayolitambulisha shirika, katiba ya shirika na Cheti cha usajili.
Ili kuhakikisha NGO’S zitafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu shirika linawajibika kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zake kwa kila robo mwaka.
Pia Halmashauri kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii huakikisha inafanya mkutano wa NGO’S kadri rasilimali zinavyopatikana.
Hadi sasa halmashauri ya wilaya ya Masasi inafanya kazi na Mashirika 52.