• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Utawala na Rasilimali Watu

UTANGULIZI

Idara ya Utawala na Utumishi ni Idara pana inayojumuisha ngazi za Vijiji Kata, tarafa na Halmashauri makao makuu. Hadi sasa halamashauri ya wilaya ya masasi ina jumla ya vijiji 166 na Kata 34 na tarafa 5 ambazo ni Mchauru, Chiungutwa, Chikundi, Lisekese B na Lulindi.

UTUMISHI;

Ofisi ya Utumishi Ina jumla ya Maafisa Utumishi 6 na Mkuu wa Idara 1. Idara hii ina majukumu mbalimbali yaliyogawanywa kwa maafisa utumishi waliopo ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Kushughulikia maslahi ya watumishi kama malalamiko, kusimamia mafunzo kwa watumishi, likizo, kusimamia utendaji kazi wa watumishi kwa kusimamia kanuni, sheria, nyaraka na taratibu za utumishi wa umma katika kuhudumia umma, kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao kama mshahara wa kila mwezi, makato, mikopo kwa watumishi pamoja na kusimamia ujazaji wa fomu za OPRAS

MAJUKUMU YAMEGAWANYWA KAMA IFUATAVYO.

1. Kuratibu Mafunzo 

Idara inawajibika kuratibu na kuandaa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kwa watumishi kulingana na mahitaji ya taasisis lakini pia kama haki ya mtumishi kuongeza elimu akiwa mahali pa kazi. Utaratibu wa kwenda kwenye mafunzo hayo huanzia katika Idara husika baada ya mtumishi kufanyiwa tathmini ya utendaji kazi wake pamoja na elimu aliyonayo, Idara huamua kumuweka mtumishi katika bajeti ili aweze kuhudhuria mafunzo au masomo kulingana na mahitaji na mapungufu aliyonayo. Utaratibu huu unatokana na matokeo ya kujaza fomu za Opras ambapo changamoto za utendaji kazi huonekana katika fomu hizo.Hata hivyo Maombi ya kuingia kwenye mpango wa mafunzo yanaanzia Januari hadi Machi ya kila mwaka.

2. Kuratibu Likizo 

Idara inaratibu likizo zote za watumishi wa halmashauri.
Watumishi wote wanatakiwa kujua kwamba likizo ni haki yao na ni muhimu kwao.Pia wanapaswa kujua kuwa utaratibu wa kwenda likizo huanzia kwenye Idara husika kwa Wakuu wa Idara kuandaa mzunguko wa likizo (Leave Roster) ya kila mtumishi kulingana na tarehe yake ya ajira . Pia wanapaswa kujua likizo za watumishi zinapitishwa kulingana na Leave Roster iliyowasilishwa. Aidha ijulikane pia kuna likizo ya malipo ambapo mtumishi anastahili nauli kwake na familia yake ikiwemo mke/mume, watoto wasiozidi wanne chini ya umri wa miaka18. Na iombwapo inatakiwa iwe na viambatanisho ambavyo ni cheti cha ndoa na vyeti vya kuzaliwa vya watoto na sio “Affidavit.”

3. Upimaji Utendaji kazi wa wazi (OPRAS) 

Idara pia inaratibu zoezi la Upimaji Utendaji kazi wa wazi yaani OPRAS kwa watumishi. Opras ni muhimu kwa watumishi kwenda kozi kwani ni kigezo kimojawapo cha upandaji cheo, na pia inaonyesha mapungufu ya Mtumishi kwa hitaji la kwenda masomoni, inaleta ufananisi katika kutekeleza majukumu, inaleta ushirikiano n.k. Zoezi la Opras hufanyika kila mwanzo wa mwaka wa Serikali yaani July ambapo watumishi wote wanatakiwa kujaza malengo yao ya mwaka katika fomu hizo baada ya kukubaliana na wasimamizi wao wa kazi. Aidha ifikapo Desemba wanatakiwa kufanya mapitio ya nusu mwaka wakieleza utekelezaji wa malengo yao ulipofikia na kama kuna mabadiliko yoyote ya malengo wanaweza kuyarekebisha hapa. Pia ifikapo mwisho wa mwaka yaani Juni kila mtumishi anatakiwa kueleza utekelezaji wa malengo aliyojiwekea mwanzo wa mwaka amefanikisha kwa kiwango gani halafu anatakiwa ajipime pia apimwe na msimamizi wake wa kazi. Kwa mwaka wa fedha 2015/16 watumishi zaidi ya 90% wamefanikisha kujaza fomu za OPRAS na wameanza kuelewa umuhimu wa fomu hizo.

4. Mikopo ya Watumishi (1/3 ya Mshahara)

Watumishi wanatakiwa kujua kwamba unapokopa unatakiwa ubaki na I/3 ya mshahara wako na kwamba mikopo yote inaingizwa kupitia system ya LAWSON ili makato yaweze kukatwa kila mwezi.

5. Kushughulikia malimbikizo ya Watumishi 

Watumishi wote wanatakiwa kujua kuhusu utaratibu mpya wa malimbikizo (arrears). Mtumishi yeyote aliepanda cheo na akachelewa kurekebishiwa mshahara akawa na madai ya malimbikizo au ajira mpya aliechelewa kupata mshahara akawa anadai malimbikizo haitaji kujaza fomu za malimbikizo (arrears) kwa sababu kwa sasa malimbikizo (arrears) yanalipwa moja kwa moja. Hivyo anachotakiwa kufanya ni kwenda kwa Afisa Utumishi anaeshughulika na malimbikizo (ARREARS) na kuona kama madai yako yatalipwa moja kwa moja au kuna shida yeyote.

6. KURATIBU VIKAO VYA KISHERIA

Idara inaaratibu vikao vyote vya kisheria kuanzia ngazi ya kijiji (mkutano mkuu wa kijiji), kata na Halmashauri zikiwemo vikao mbalimbali vya kamati za kudumu za halmashauri na vikao vya bodi mbalimbali.

7. KUPANDISHA VYEO WATUMISHI

Idara inawajibika kupandisha vyeo watumishi kwa mujibu wa miundo na sheria Na. 8 ya mwaka 2002 na kanuni ya utumishi wa umma ya mwaka 2003. Mtumishi anaweza kupanda cheo akiwa ni mwadilifu, mchapakazi, awe na utendaji kazi mzuri (utendaji unaoleta matokeo chanya kwa taasisi) pia awe na ametumikia cheo husika kwa muda wa miaka mitatu pamoja kujaza OPRAS.

8. KUSHUGHULI MASUALA YA NIDHAMU KWA WATUMISHI.

Idara inawajibika kusimamia masuala ya nidhamu kwa watumishi kwa kizingatia sheria na kanuni za kudumu za utumishi wa umma ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2003, pamoja na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004. Kwa sheria hii idara inawaibika kushughulikia masuala ya nidhamu kwa watumishi wote isipokuwa watumishi wa idara ya elimu msingi na sekondari ambao mamlaka yao ya nidhamu ni Tume ya Utumishi ya Walimu (TSD) iliyoanzishwa na sheria Na. 8 ya mwaka 2002.

Mojawapo ya makosa ambayo mtumishi anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni kama utoro kazini, rushwa, kuto tii mamlaka, kumsababishia hasara mwajiri, ulevi, kutoa taarifa za siri za serikali, kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma pamoja na maadili taaluma, kushindwa kutekeleza majukumu uliyopangiwa

9. KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO 

Idara inaratibu malalamiko kupitia dawati la malalamiko, ambapo malalamiko yanayopokelewa yanashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo na hii imesaidiaa kupunguza malalamiko kwenye taasisi

  • MALENGO YA IDARA  KATIKA UTOAJI WA HUDUMA 

                   Idara  hii  ina Malengo yafuatayo katika Utoaji huduma

  • Kuhakikisha Misingi  ya Utawala Bora inatekelezwa katika Halmashauri. Misingi hiyo ya Utawala Bora ni kama ifuatavyo. Misingi ya Utawala Bora  inatekelezwa . Misingi hiyo ni kama ifuatavyo:-
  • Utawala wa Kidemokrasia
  • Utawala wa Sheria
  • Ushirikishwaji  wa Umma
  • Haki na Usawa kwa Watu wote
  • Uwajibikaji katika Utendaji
  • Uwazi katika uendeshaji Shughuli
  • Uadilifu
  • Kukidhi matakwa ya Wananchi.

( b)  Kuhakikisha Halmashauri  inapata  Watumishi bora wanaohitajika  katika sekta zote za    kutoa huduma  kwa Wananchi ,kama vile Sekta ya Afya, Sekta ya Elimu na Sekta ya Kilimo.

Watumishi hao wawe na  Maadili ya Utendaji yafuatayo:-

  • Kutoa Huduma Bora
  • Utii   kwa Serikali
  • Bidii ya Kazi
  • Kutoa huduma bila Uperndeleo
  • Kufanya kazi kwa  Uadilifu
  • Kuwajibika kwa Umma
  • Kuheshimu Sheria
  • Matumizi sahihi ya Taarifa.
  • VITENGO VILIVYOPO KATIKA IDARA NA MAJUKUMU YAKE:
  • Idara hii ina Vitengo viwili. Vitengo hivyo ni
  • Utawala
  • Utumishi.
  • Majukumu ya Vitengo
  • Majukumu ya kitengo cha Utawala ni kuratibu Shughuli za Utawala Bora kwa Wananchi.
  • Majukumu ya kitengo cha Utumishi ni kushughulikia Masuala ya  Ajira ,Maslahi,Mafunzo
  • na  Nidhamu za Watumishi wa Umma katika Halmashauri.

3  MAJUKUMU YA IDARA

( a)  Kuratibu Shughuli za   utawala Bora katika Halmashauri .

(b) Kusimamia Ajira za Watumishi katika Halmashauri.

 ( c ) Kushughulikia Maslahi ya Watumishi ili waweze kutoa huduma bora kwa 

          Wananchi.

      (d ) Kushughulikia Mafunzo kwa Watumishi  ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma

              bora kwa   ufanisi.

      (e)    Kusimamia na kushughulikia  masuala ya nidhamu ya Watumishi.

4: AINA ZA HUDUMA MUHIMU ZINAZOTOLEWA KWA JAMII MARA KWA MARA

  ( a ) kusimamia ufanyikaji wa vikao vya kisheria vya Halmashauri ya wilaya.

  (b) Kusimamia Ufanyikaji wa  vikao vya Halmashauri za vijiji na Mikutano mikuu ya Vijiji kwa mujibu wa

        Sheria

 ( C)  Kupokea Malalamiko na maoni mbalimbali ya Wananchi na kuyafanyia  kazi.

 (d) Kusimamia Utekelezaji wa  Sheria ndogo katika ngazi ya Halmashauri ,kata na vijiji.

(e) Kuhakikisha Watumishi wanatoa huduma Bora kwa Wananchi.

5; IDADI YA WATUMISHI

Idara ya Utumishi na Utawala ina Watumishi 178 . Kati ya Watumishi hao, watumishi 52 wapo makao makuu na Watumishi 127 ni watendaji kata na Vijiji  ambao wapo katika kata 34 za Halmashauri.

Mkuu wa Idara        :   Festo  J. Mwangalika       Simu :   0658973113

Maafisa Utumishi :       1.   Majid Luwo                   Simu   0784423096

                                    2     Rehema Yusuph         Simu  0788812981

                                    3     Julia Anthony              Simu  0752187155

                                    4. Nelson J. Nkamba          Simu  0682694651

                                    5. Huhudi O. Nkwama         Simu  0715933104

                                            

6: MIONGOZO NA SERA MBALIMBALI INAYOTUMIWA NA IDARA NA VITENGO

     KATIKA  KUTEKELEZA MAJUKUMU YA KILA SIKU.

      (i)Sheria ya Seikali za Mitaa(Mamlaka ya Wilaya) Namba 7 ya mWaka 1982.

      (ii) Sheria ya Fedha za Serikali za mitaa, Namba 9 ya Mwaka 1982

  •  Sheria ya Utumishi wa Umma, Namba 8 ya Mwaka 2002
  • Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba  5 ya Mwaka 1999
  • Sheria ya Mabaraza ya Kata Namba 7 ya Mwaka 1985
  • Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Namba 4 ya Mwaka 1979.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa